Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chombo kinachosimamia utekelezaji wa Programu zinazofadhiliwa na Global Fund ( Tanzania National Coordinating Mechanism - TNCM) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha wajumbe wa chombo hicho kwaajili ya kujadili utekelezaji wa program za Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI pamoja na uimarishaji wa mifumo ya kutolea huduma za Afya Nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kipindi cha kuanzia mwaka 2024 hadi 2026.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 9 Agosti, 2024 katika Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment