Na Saida Issa,Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul leo Agosti 29,2024 bungeni jijinj Dodoma ameibana
Serikali ieleze ina mpango gani wa kuwalipa fidia Wananchi wa Babati waliopisha ujenzi wa barabara za mchepuko takribani miaka minne sasa iliyopita.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa ujenzi Godfrey Kasekenya amesema baada ya Usanifu wa Kina na Uthamini wa mali zitakazoathiriwa na mradi wa barabara ya mchepuo wa Mji wa Babati (Babati Bypass), tathmini ilionesha kwamba barabara pendekezwa ya ’Babati Bypass’ (km 27) inapita katika maeneo ya Mji wa Babati yenye nyumba nyingi na kusababisha gharama ya fidia kuwa kubwa kiasi cha shilingi bilioni 9.05.
Kasekenya amesema kuwa Kutokana na hali hiyo, Serikali imemuelekeza Mhandisi Mshauri kupendekeza njia nyingine mbadala ambayo itapita nje ya Mji, hivyo, fidia kwa njia ya awali imesitishwa.
No comments:
Post a Comment