Marekani jana Alhamisi ilitangaza kuidhinisha mauzo ya makombora 600 ya Patriot yenye thamani ya dola bilioni 5 pamoja na vifaa vingine nchini Ujerumani.
Shirika la Ushirikiano wa Usalama wa Ulinzi (DSCA) limesema makombora hayo aina ya PAC-3 MSE yataimarisha uwezo wa Ujerumani wa kukabiliana na vitisho vya sasa na baadae na kuboresha uwezo wa kiulinzi wa jeshi lake na la Jumuiya ya NATO.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliidhinisha mauzo hayo ya makombora kwa Ujerumani na DSCA jana Alhamisi ililiarifu Bunge, ambalo pia linatakiwa kuidhinisha.
Ujerumani imeisaidia Ukraine mifumo kadhaa ya Patriot, katikati ya mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu yake na hivyo kuhitaji msaada zaidi wa kujilinda.
No comments:
Post a Comment