Akiwa na umri wa miaka 37, Shinawatra, atakuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi nchini humo na mwanamke wa pili kuwahi kushikilia wadhifa huo baada ya shangazi yake Yingluck.
Wabunge wamemuidhinisha Paetongtarn wa chama cha Pheu Thai kuwa waziri mkuu kwa kupata kura 319 dhidi ya 145 waliopinga. Kuchaguliwa kwake kunatokea siku mbili tu baada ya Waziri Mkuu wa zamani Srettha Thavisin kuondolewa na mahakama ya kikatiba.
Waziri Mkuu huyo mpya anakabiliwa na kibarua kigumu cha kufufua uchumi wa Thailand na kuepuka mapinduzi ya kijeshi na uingiliaji kati wa mahakama ambao umeondoa tawala nne zilizopita.
No comments:
Post a Comment