MBUNGE CHEMBA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KATIKA KATA YA HANDA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 11, 2024

MBUNGE CHEMBA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI KATIKA KATA YA HANDA


 Na Saida Issa, Dodoma 

MBUNGE wa Chemba Mhe.Mohammed Moni amekabidhi mifuko 50 ya saruji kwaajili ya kumalizia ofisi ya kijiji cha handa pamoja na mifuko 50 yakuanzisha ujenzi wa zahanati katika kijiji hicho. 


Akizungumza alipokuwa akikabidhi mifuko hiyo alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi. 


"Nina kila sababu ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa ni chachu ya maendeleo kwa kuhakikisha kila kata inapata pesa za miradi namimi kama Mbunge wa chemba namuahidi sitamuangusha bali nitahakikisha fedha hizo zinatumika katika matumizi yaliyokusudiwa,"amesema. 


Amesema kuwa fedha walizopokea ni pamoja na zaidi ya shilingi Milioni 500 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi,zaidi ya milioni 300 kwaajili ya umaliziaji wa shule ya sekondari na shilingi Milioni 53 ni kwa ajili ya madarasa na matundu ya vyoo shule ya msingi Handa A.

No comments:

Post a Comment