WAKAZI wa Kijiji Cha Mkunguwakihendo na Kata ya Kikio wapo mbioni kuondokana na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan kutoa fedha zaidi ya Sh Milioni 395.9 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji.
Kukamilika kwa mradi huo kutaongeza upatikanaji wa maji hadi asilimia 65 kutoka asilimia 53 waliyonayo sasa kiwilaya.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Agosti 18,2024,Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu amesema ameridhishwa na kazi ya utekelezaji wa mradi huo.
Amesema ujenzi wa mnara wa mita sita umekamilika na Sasa wanajiandaa kumwaga zege la kitako cha tenki kisha wajenge tenki ambapo kwa ujumla mradi unakadiriwa kutekeleza kwa asilimia 65.
"Ninafarajika kuona muda sio mrefu wananchi wa Mkunguwakihendo na Kata ya Kikio kwa ujumla wanaenda kumaliza changomoto waliyonayo ya kupata maji safi na salama tokea Dunia iumbwe,kwa niaba ya wananchi wangu tunaendelea kumshukuru Rais wetu Samia kwa kututengea fedha nyingi za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya Maji,".ameshukuru.
Mwishoni mwa mwezi Julai Mwaka huu Mbunge Mtaturu alifanya ziara kwenye eneo la mradi na kuukuta mradi ukiwa kwenye asilimia 25 ya ujenzi na hivyo alimtaka Meneja wa Ruwasa Ikungi kuongeza kasi ili wananchi wanaotaabika kwa kukosa maji ilhali Serikali ya Awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeshatenga fedha za mradi huo waweze kupata maji.
Malengo yaliyopo kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025 ni kuhakikisha maji yanafika kwa asilimia 85 Vijijini na asilimia 95 Mijini ifikapo 2025.
Katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa kampeni ya kumtua Mama ndoo ya maji kichwani inaenda kwa kasi.
#SamiaTunatambaNaye#2025TunaendaNayeSingidaMashariki#
No comments:
Post a Comment