TETESI ZA USAJILI ULAYA AGOSTI 13,2024 "VINICIUS JR ANASAKWA NA LIGI KUU YA SAUDIA" - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 13, 2024

TETESI ZA USAJILI ULAYA AGOSTI 13,2024 "VINICIUS JR ANASAKWA NA LIGI KUU YA SAUDIA"


Mshambuliaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 24 Vinicius Jr anasakwa na Ligi kuu ya Saudia. (ESPN)

Manchester United wamefanya majadiliano ya kina kuhusu usajili wa wachezaji kadhaa msimu huu wa joto, akiwemo Muingereza wa Everton, Dominic Calvert-Lewin, 27. (Sky Sports)

Southampton wamekubali mkataba wa pauni milioni 12.8 sawa na (euro 15m) kumuuza beki wa Ujerumani Armel Bella-Kotchap, 22, kwenda Hoffenheim, huku uchunguzi wa kimatibabu ukipangwa kufanyika Jumanne. (Sky Sports)

Napoli wamewasilisha ofa ya thamani ya euro 25m sawa na pamoja na euro milioni tano kama nyongeza ya ziada kwa mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31. (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano

Newcastle wanatafuta chaguo mbadala wa safu ya ulinzi licha ya kuwasilisha ombi la tatu la kumsajili beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24. (Athletic - usajili unahitajika)

Crystal Palace pia wanafuatilia hali ya kiungo wa Chelsea Carney Chukwuemeka, 20, na watawasilisha ombi lao ikiwa Muingereza huyo atapatikana. (South London Press)

Ombi la Bournemouth la kumnunua mshambuliaji wa Brazil Evanilson, 24, limekataliwa na Porto. (Fabrizio Romano)

Newcastle wanatazamiwa kumnunua winga wa Chelsea Muingereza Noni Madueke mwenye umri wa miaka 22 ikiwa kikosi cha Eddie Howe kitamuuza kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron, 30, kwa Charlotte FC. (ipaper)

Liverpool wamepokea ofa ya tatu kutoka kwa Red Bull Salzburg kumnunua kiungo wa kati Bobby Clark mwenye umri wa miaka 19. (Time - usajili unahitajika)

Beki wa Wales Chris Mepham, 26, anatarajiwa kuondoka Bournemouth msimu huu kwa mkataba wa kudumu au wa mkopo, huku Ipswich, Torino na Anderlecht zikiwa na nia ya kumsajili. (Fabrizio Romano)

Leicester City wamefikia makubaliano na Bayer Leverkusen juu ya mkopo na wajibu wa kumnunua mshambuliaji wao wa Jamhuri ya Czech Adam Hlozek. The Foxes bado wanahitaji kukubaliana juu ya masharti ya usajili na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Sky Germany)

Manchester United wameanzisha tena mazungumzo na Everton kuhusu kumsajili beki wao wa Uingereza Jarrad Branthwaite mwenye umri wa miaka 22 kwa pauni milioni 60. (Football Insider)

Manchester City wako tayari kumwachia kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, aondoke kwa mkopo, huku Ipswich, Everton na Fulham zikiwa na nia ya kumsajili. (Manchester Evening News)

Nottingham Forest wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Paraguay Ramon Sosa kutoka klabu ya Talleres ya Argentina. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ungekuwa na thamani ya karibu £11m. (Telegraph - usajili unahitajika)

Aston Villa, Fulham na Crystal Palace wako mbio kumsajili beki wa Chelsea Muingereza Trevoh Chalobah, 25. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Tottenham Dane Scarlett, 20, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na kalabu ya Oxford United kwa mkopo. Muingereza huyo tayari ameshacheza mechi 10 akiwa na Spurs. (Telegraph - usajili unahitajika)

No comments:

Post a Comment