Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu ametembelea Ofisi za Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) , jijini Dar es salaam.
Mhe. Sangu ametembelea ofisi hizo leo Ijumaa Septemba 13, 2024 kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala hiyo pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia TGFA
Katika ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri Sangu amepokelewa na Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Mululi Mahendeka na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi pamoja na watumishi wengine wa Wakala hiyo.
No comments:
Post a Comment