Na Said Njuki, Arusha
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Save the Children la wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha, limiitaka jamii kutowatumikisha watoto.
Kutokana na kuwepo Kwa utumikishani WA watoto kinyemela, Shirika hilo jana limetoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wafanyabiashara katika soko la Tengeru wilayani Arumeru kwa lengo la kupambana na wimbi la utumikishwaji wa watoto masokoni hivyo kuathiri masomo yao shuleni.
Akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia, Meneja wa Miradi kutoka Mkoa wa Dodoma wa Shirika la Save the Children, Mariam Mwita alisema wamefika eneo hilo, kutoa elimu hiyo ikiwa ni mwendelezo wa shughuli za Wiki ya Azaki zinazofanyika jijini hapa kwa siku tano.
Alisema wamekwenda kwenye soko hilo, kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kwa kuwa wengi wao ni wazazi na walezi wa watoto lakini utumikishwaji watoto katika soko hilo umekuwa kama jambo la kawaida.
"Tumekuwa tukiooa elimu ya ajira mbaya kwa watoto,ll lishe bora na familia lengo likiwa kuwagusa watoto ili wazazi wafanye biashara lakini wasijihusishe na Ajira dhidi ya watoto".alisema Mwita.
Aidha, aliwataka wazazi kutumia kipato wanachokipata kuboresha lishe za watoto, kuwanunulia mahitaji muhimu ikiwamo mahitaji ya shule, malazi bora na mavazi ili kuwapa mazingira mazuri yatakayowafanya kukua makuzi safi.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Meru Martha Mazava, Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Meru, alisema wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali katika soko hilo juu ya masuala ya ajira kwa watoto, afya, kilimo na uwezeshaji wa kundi hilo kiuchumi.
"Uchumi wa wananchi ukiimarika watoto wataondokana na ukatili wa kijinsia kwa kuwa watapata mahitaji yao ya msingi ikiwamo chakula, mavazi na malazi...tutaendelea kufanya hivyo kwa faida ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Alisema katika hatua ya kukabiliana na matukio hayo,wanatoa elimu ngazi za kata, kwenye mikutano ya vijiji,pia wameunda Kamati za Kupambana na Kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA).
"Kamati hizi ziko kwenye kata zote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwenye vijiji vyote 60 kwa kuwa mpango mkakati wetu ni kupinga na kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto,"alisisitiza.
No comments:
Post a Comment