WAZIRI DKT. GWAJIMA, BALOZI MPYA IRELAND WAZUNGUMZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 12, 2024

WAZIRI DKT. GWAJIMA, BALOZI MPYA IRELAND WAZUNGUMZA


Na WMJJWM, Dar Es Salaam


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Ireland nchini, Mhe. Nicola Brennan aliyetembelea ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam Septemba 12, 2024 kwa lengo la kujitambulisha.

Katika mazungumzo yao Waziri Dkt. Gwajima amemueleza Balozi Nicola mafanikio, changamoto na maeneo ya kufanyia kazi pamoja hususani eneo la Jinsia.

Naye Balozi Nicola amesema kuwa, eneo la Jinsia ni kipaumbele kwa hasa katika kuwawezesha wanawake kwenye maeneo ya vijijini kujikwamua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment