MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA KUISHI NJE YA KITUO CHA KAZI KATIKA HALMASHAURI MAELEZO YA PICHA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 3, 2024

MARUFUKU WATUMISHI WA UMMA KUISHI NJE YA KITUO CHA KAZI KATIKA HALMASHAURI MAELEZO YA PICHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia na kumpatia ndoo ya maji mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mara baada ya kukagua na kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Kemakorere Nyarero wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Sehemu ya Wananchi wa wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Koryo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Sehemu ya wazee wa mila na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichan) wakati akizungumza nao alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa na Viongozi na Watendaji wa Wilaya ya Rorya wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa kabla ya Waziri huyo, kukagua na kuzindua Shule ya Msingi Komote wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifungua maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime baada ya kukagua mradi huo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo mkoani Mara kwa lengo la kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikata utepe kuzindua Shule ya Msingi Komote iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.

No comments:

Post a Comment