Mwandishi Wetu ,Manyara .
Kampuni ya kuzalisha Vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imeibuka kinara katika maonyesho ya Biashara ,Viwanda na Kilimo ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 baada ya kushinda Tuzo ya wazalishaji bora wa vinywaji changamshi miongoni mwa makampuni yaliyoshiriki kwenye maonyesho hayo kutokana na ubora wa bidhaa wanazozilisha kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo 4 za wazalishaji bora , wafanyabiashara bora ,banda bora pamoja na mshindi wa jumla.Meneja Masoko na Mauzo kutoka kampuni ya Mati Super Brand Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuhakikisha kuwa inazalisha bidhaa bora zinazouzika katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo mbali na kushiriki kwenye maonyesho imekua ikidhamini maonyesho hayo kwa mara 3 mfululizo kwa lengo la kuunga mkono TCCIA Manyara na Serikali kwa kuwawezesha wajasiriamali kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao na kupata masoko.
"Kwa Muda mrefu tumekua ni wadau wa maendeleo kwa mkoa wa Manyara tukishirikiana na serikali katika ngazi mbali mbali na kwa namna tofauti katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo ujasiriamali ,viwanda na biashara " Anaeleza Mpoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Manyara Musa Msuya ameipongeza Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kudhamini maonyesho hayo kila mwaka
Katibu wa TCCIA Zainab Rajab amesema kuwa maonyesho hayo yamekua na mafanikio makubwa kwa wajasiriamali kwani wameweza kutangaza bidhaa zao na kupata fursa za masoko.
No comments:
Post a Comment