"Waziri Mavunde Atoa Viti Mwendo kwa Watu Wenye Ulemavu Dodoma" - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 30, 2024

"Waziri Mavunde Atoa Viti Mwendo kwa Watu Wenye Ulemavu Dodoma"



Na Okuly Julius _Dodoma


Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde, amekabizi vifaa saidizi vya watu wenye ulemavu, ikiwemo Viti mwendo 20 kwa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu na wanachi wengine.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Viti mwendo hivyo leo Oktoba 30,2024 jijini Dodoma Mavunde amesema kuwa watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto ya kutoka eneo moja kwenda lingine hivyo Ofisi yake imeona sababu ya kuendelea kutoa visaidizi hivyo ili kuwarahisishia katika utekelezaji wa majukumu yao.

"mimi na Ofisi yangu tuna tabia kila mwaka wa kufanya hivi kwa kutoa chochote kwa watu wenye ulemavu na leo tunatoa hapa kwa SHIVYAWATA ili wao watusaidie kufikisha kwa wanafunzi wenye ulemavu na wananchi wengine wenye uhitaji, tunaamini itakwenda kuwasaidia katika majukumu yao, "amesema Mavunde

Mavunde amesema ataendelea kushirikiana na Viongozi wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa kama watu wengine ikiwemo katika.

"tuna asilimia mbili ya Mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ni kama sehemu ya mikopo kwa watu wenye ulemavu tunaamini kabisa sisi kama Serikali tukishirikiana na viongozi wao tutahakikisha fedha hizi zinawafikia na vifaa hivi vikawe chachu katika maisha yao ya kila siku, "ameeleza Mavunde

Naye Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma Omary Luvuva
amesema vifaa hivyo vinakwenda kuwasaidia watoto wenye ulemavu katika eneo la Elimu na pia katika kufuata huduma nyingine na kuzifuata fursa mbalimbali.

" vifaa hivi ni msaada mkubwa katika kuhakikisha watoto wenye elimu wanaipata fursa ya elimu ipasavyo na katika mazingira ambayo ni rafiki," ameeleza Luvuva

Mbunge wa Viti Maalumu Hadija Shaaban Taya ametoa wito kwa Wabunge wengine kuiga mfano wa Mavunde katika kuwasaidia watu wenye ulemavu katika majimbo yao.




No comments:

Post a Comment