IGHONDO ALETA MAKOCHA KUTOKA NJE YA NCHI, WATOA MAFUNZO FOUNTAIN GATE DODOMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 31, 2024

IGHONDO ALETA MAKOCHA KUTOKA NJE YA NCHI, WATOA MAFUNZO FOUNTAIN GATE DODOMA.

 


Na Saida Issa, Dodoma 

MBUNGE wa  jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo, ametoa mafunzo kwa makocha na walimu wa michezo wa shule za Mkoa wa Dodoma kutoka kwa Walimu wa makocha aliyowatoa Nchini Sweden lengo likiwa ni kuiibua na kukuza vipaji kwa vijana wenye umri wa miaka 5-19.


Mafunzo yamefanyika  jana jijini Dodoma, katika shule ya msingi na sekondari ya fountain gate. 


Ighondo alisema lengo lake haswa yale magoli yanayolipiwa milioni 5 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yaanze kutokea Singida. 


"Tanzania sisi ni nchi tajiri hata ukiingia katika sekta ya michezo utaona namna Mama yetu Dkt. Samia anavyo thamini vipaji na analipa kila gori sasa nataka kuwahakikishia kwamba fedha hizo zitakuja jimboni kwangu kwani nimejipanga kutomuangusha Rais wetu, 


Licha ya kuwepo mkoa wa Singinda kwa siku mbili leo pia wamekuja kutoa fulsa kwa mkoa wa dodoma pamoja na shule hii kwaajili ya kuhakikisha tunaibua na kukuza vipaji vya vijana wa umri wa miaka 5 kwenda juu mpaka miaka 19,"alisema.


Kwa upande wake Joseph Mjingo mwalimu wa Taaluma shule ya Fountain gate alimshukuru mbunge wa jimbo la singida kaskazini kwa kuona na kutambua thamani ya shule hiyo wanachokifanya.


"Ujio wa walimu wa makocha na walimu wa michezo katika shule yetu ni jambo nzuri na kubwa sana kwani sisi Faunten get naweza kusema ndio taasisi pekee Tanzania hii ambayo unaweza ukapata timu za aina zote kuanzia watoto wa miaka 3 na kuendelea lakini vile vile utapata timu za kuanzia miaka 5 na kuendelea,"alisema.


Pia alisema kuwa wao wanaendelea kushirikiana na wadau wote wenye nia njema na Taifa hasa katika suala la michezo na kuwaongezea chachu ya kuwapika watoto kwaajili ya kesho yao.


Naye Mwalimu Gaston kusenha ambaye ni mwalimu wa michezo kutoka shule ya Brother Marthin akiwa ni miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo alisema kuwa ushiriki wake katika mafunzo hayo utawasaidia walimu wa michezo kuwafundisha wanafunzi na waweze kupata uzoefu kuanzia wakiwa wadogo huku akitamani program hiyo iende na katika maeneo ambayo bado haijafika.







No comments:

Post a Comment