MBUNGE NJEZA AIBANA SERIKALI JE, LINI UZALISHAJI WA MADINI YA NIOBIUM NA KIWANDA CHA FARRONIOBIUM UTAANZA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA? - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 31, 2024

MBUNGE NJEZA AIBANA SERIKALI JE, LINI UZALISHAJI WA MADINI YA NIOBIUM NA KIWANDA CHA FARRONIOBIUM UTAANZA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA?

 


Na Saida Issa, Dodoma 

NAIBU waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amesema kuqa kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura 123, wamiliki wa Leseni za Kati na Kubwa za uchimbaji Madini wamepewa sharti la kutoa hisa huru na zisizofifishwa zisizopungua asilimia 16 kwa Serikali.


Hayo ameyaeleza Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Mbeya Vijijini Oran Njeza alipouliza Je, lini uzalishaji wa Madini ya NIOBIUM na kiwanda cha Farroniobium utaanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.


Amesema kuwa Kutokana na uwepo wa takwa hilo la kisheria, Serikali ilianza majadiliano na kampuni ya Panda Hill kwa lengo la kusaini Mkataba wa Makubaliano utakaowezesha Serikali kupata umiliki wa hisa hizo kwenye mradi huo ikiwa ni pamoja na manufaa mengine ya kiuchumi. 


"Mradi wa uchimbaji wa madini ya niobium katika eneo la Panda Hill, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya unamilikiwa na kampuni ya Panda Hill Tanzania Limited (PHTL) ambayo ina leseni tatu za uchimbaji wa kati wa madini (Mining Licence) kwa ajili ya kuzalisha mazao mbalimbali ya madini,

Moja ya mazao ya madini ya niobium baada ya kuyachakata ni ferroniobium,


Zao hili hutumika kwenye injini za ndege na rockets, mitambo ya uchorongaji ya utafiti wa mafuta (oil rigs), mabomba ya gesi na mafuta, pamoja na utengenezaji wa magari kutokana na sifa ya kuzuia mitambo husika kushika kutu,"amesema. 


Kadhalika amesema kuwa Majadiliano hayo bado yanaendelea na yapo katika hatua nzuri.


Serikali iko mbioni kukamilisha majadiliano hayo sambamba na kukamilika kwa taratibu za ulipaji wa fidia wananchi wa eneo husika ili kuwezesha shughuli za uchimbaji na ujenzi wa kiwanda cha ferroniobium kuanziasha,"amesema.

No comments:

Post a Comment