Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti baada ya kuzindua Zahanati ya Getarungu iliyopo kata ya Nyansurura wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi akitoa neno la shukrani kwa Serikali kutokana na miradi ambayo imeitekeleza katika mkoa wake wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Baadhi ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyesimama kushoto) wakati akizungumza nao baada ya kukagua na kuzindua Zahanati ya Wilaya ya Serengeti wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Mwonekano wa vitanda vya wagonjwa vitakavyotumika katika Zahanati ya Getarungu iliyokaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene katika Zahanati ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo baada ya kukagua vitanda vya wagonjwa kwenye Zahanati ya Getarungu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakati wa ziara yake ya kikazi katika mkoa wa Mara iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyevaa miwani) akisikiliza changamoto ya kiutumishi kutoka kwa Mhe. Diwani Bw. Josephat Seronga (aliyevaa kofia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwonekano wa nyumba wa Zahanati ya Getarungu iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambayo imekaguliwa na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa ziara yake ya kikazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambayo aliikagua na kuizindua wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Bi. Kemirembe Lwota baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo kwa lengo la kukagua na kuzindua Zahanati ya Getarungu iliyopo katika Halmashauri hiyo mkoani Mara.
Na. Veronica Mwafisi-Serengeti
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi wa Mkoa wa Mara kutekeleza miradi ya maendeleo kwa usahihi ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kutumika kikamilifu na wananchi.
Akizindua mradi wa Zahanati ya Getarungu uliofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani kupitia Shirika ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) tarehe 3 Oktoba, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto za wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa zahanati hiyo na kutaka halmashauri za mkoa huo kuiga utekelezaji wa namna hiyo.
“Nimefurahi sana, kupitia ziara hii nzuri, kubwa nililojifunza ni utekelezaji wa miradi kwa usahihi sana, tujifunze na sisi halmashauri kuangalia miradi inayotekelezwa kwa usimamizi mzuri inavyokuwa na je sisi tunashindwa wapi? Mhe. Simbachawene ameuliza
Amesema mradi huo wa zahanani ya Getarungu umesimamiwa na Mkandarasi Maalum na umekuwa ni wa kuridhisha sana, lakini kwenye halmashauri ambako Wakandarasi wanalipwa mishahara, miradi yao inakuwa sio ya kuridhisha.
“Nimezindua zahanati hii ya Getarungu kwa kujidai sana, ni nzuri inafurahisha, nawasisitiza viongozi katika halmashauri kuiga mfano huu mzuri, tukiendelea kutosimamia kwa usahihi tutachukuliana hatua. Mhe. Simbachawene amesisitiza
Amesema utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya jitihada za kukuza sekta ya utalii, kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii na kujenga mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo na ndio sababu ya kupatikana kwa mradi huu wa zahanati 8 kwa mara moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ikiwemo hiyo aliyoizindua leo ya Getarungu.
Mhe. Simbachawene ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika Mkoa wa Mara, ambapo leo ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Butiama na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo zahanati ya Getarungu, barabara ya kituo kipya cha mabasi Koreri na Shule ya Msingi Chief Manyori.
No comments:
Post a Comment