PURA Yafanya Ziara ya Ufuatiliaji Eyasi-Wembere - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 16, 2024

PURA Yafanya Ziara ya Ufuatiliaji Eyasi-Wembere


Katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria, Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imefanya ziara ya ufuatiliaji katika Kitalu cha Eyasi Wembere ambako kazi ya uchukuaji wa data za mitetemo za 2D za nyongeza (Infill and Additional 2D seismic data) inaendelea. Awali, data za mitetemo za 2D katika Kitalu hicho zilichukuliwa mwaka 2023.

Kazi ya uchukuaji wa data za nyongeza katika Kitalu cha Eyasi-Wembere ni mwendelezo wa programu ya utafutaji wa mafuta katika Kitalu hicho.

Uchukuaji wa data hizo utawezesha upatikanaji wa taarifa za kutosha kuhusu jiolojia ya Kitalu hicho. Taarifa hizo zitawezesha, pamoja na mambo mengine, uainishwaji wa maeneo ya kuchimba visima vya utafutaji wa mafuta.

Kazi ya uchukuaji wa data inatekelezwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupitia kampuni ya African Geophysical Services Limited (AGS). Hadi wakati wa ziara, utekelezaji wa kazi ulikuwa umefikia asilimia 20.

Kitalu cha Eyasi Wembere kinapatikana kaskazini mashariki mwa Tanzania katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki, tawi la Mashariki. Kitalu kina ukubwa wa kilomita za mraba 10,634.9. Eneo hilo limegusa mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu and Arusha.


No comments:

Post a Comment