WAZIRI BASHUNGWA AANZA ZIARA MAALUM MKOANI PWANI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 8, 2024

WAZIRI BASHUNGWA AANZA ZIARA MAALUM MKOANI PWANI.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb) amewasili Mkoani Pwani na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge kuanza ziara maalum ya kukagua utekelezaji na kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi leo tarehe 08 Oktoba, 2024.

Katika ziara hiyo Mfululizo katika wilaya za mkoa wa Pwani, Waziri Bashungwa leo ataanza wilaya Kibaha ambapo ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Msangani, ataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Mabweni Shule Mpya ya Viziwaziwa, atakagua ujenzi wa Soko la Halmashauri ya Kibaha, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na Miundombinu yake pamoja na kuzungumza na wananchi.

No comments:

Post a Comment