Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent L. Bashungwa akizungumza na Wananchi Kitongoji cha Karungu, kijiji cha Kanoni wilaya ya Karagwe katika mkutano wa kampeni ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, leo tarehe 23 Novemba 2024.
Katika Mkutano huo, Bashungwa ameeleza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kata ya Kanoni ambayo ni pamoja na Ujenzi wa kituo cha afya Kibona, ujenzi wa Shule mpya ya msingi Bashungwa, Ujenzi wa Shule maalum ya Wasichana ya kidato cha Kwanza hadi cha Sita pamoja na miradi mbalimbli ya barabara, maji na umeme.
No comments:
Post a Comment