Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi fedha kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga
#Amwaga Vibunda Kununua Kila Goli
# Tayari Kanunua Magoli Matano
# Kuwapa Kila Mwezi 3,500,000 /-
#Fedha kipindi cha usajili wa dirisha dogo
Na Mwandishi wetu - Shinyanga
Ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo, Mhandisi James Jumbe, mmoja wa wadau wakubwa wa michezo mkoani Shinyanga, ameahidi kutoa motisha kwa timu ya Stand United 'Chama la Wana', ambayo inashiriki Ligi ya Championship.
Mhandisi Jumbe ameahidi kununua kila goli litakalo fungwa na timu hiyo kwa kiasi cha shilingi laki mbili, huku pia akiahidi kuchangia jumla ya shilingi milioni tatu na laki tano kila mwezi kwa timu hiyo.
Mhandisi Jumbe ametoa motisha hiyo leo, Jumatatu Novemba 25, 2024, wakati akikabidhi jumla ya shilingi milioni 3.5 kwa timu ya Stand United inayoshiriki Ligi ya Championship, pamoja na shilingi milioni moja kama sehemu ya kununua magoli yaliyofungwa na timu hiyo katika michezo yake miwili ya hivi karibuni.
Magoli hayo aliyoyanunua kila moja shilingi 200,000/= ni pamoja na yale yaliyofungwa dhidi ya timu ya African Sport (goli mbili) Mkoani Morogoro na mchezo mwingine dhidi ya Mbeya City, uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage, ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli tatu kwa tatu.
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi shilingi Milioni 1 magoli matano yaliyofungwa kwa Timu ya Stand United.
"Timu ya Stand United ni nembo ya Shinyanga, tunajivunia kuwa na Stand United, ambayo imeonyesha uwezo mkubwa uwanjani. Katika mchezo wetu wa leo dhidi ya Mbeya City, tumetoka sare ya kufungana goli tatu kwa tatu. Kama nilivyowaahidi awali, kila goli litakalofungwa na timu ya Stand United, nitalinunua kwa shilingi laki mbili na kila mwisho wa mwezi nitachangia kiasi cha shilingi milioni tatu na laki tano kwa timu hii, ili kuongeza hamasa na kusaidia timu kufanya vizuri zaidi.
Leo, nakabidhi shilingi milioni moja kwa ajili ya magoli matano yaliyofungwa na timu yetu, ikiwa ni pamoja na magoli matatu yaliyofungwa dhidi ya Mbeya City na magoli mawili yaliyofungwa ugenini dhidi ya timu ya African Sport mkoani Morogoro," amesema Mhandisi Jumbe.
Mhandisi Jumbe amesema kuwa hatua hii ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo nchini.
Amesema kuwa motisha hiyo itasaidia kuongeza morali kwa wachezaji na kuchochea mafanikio zaidi kwa timu ya Stand United, ambayo ni nembo ya Shinyanga.
Motisha kwa Goli na Msaada wa Kifedha kwa Timu
"Timu yetu ya Stand United imeonyesha juhudi kubwa uwanjani, na mimi kama Mwanashinyanga, nitaendelea kuunga mkono kwa kununua kila goli linalofungwa na timu hii. Kila goli litakalo fungwa na timu yetu, nitalinunua kwa shilingi laki mbili," amesema Mhandisi Jumbe.
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe (kushoto) akikabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 3.5 kwa Timu ya Stand United.
Ameongeza kuwa pia atakuwa akitoa msaada wa kifedha wa shilingi milioni tatu na laki tano kila mwezi kwa timu hiyo ili kuongeza hamasa na kuunga mkono juhudi zao katika Ligi ya Championship, na hivyo kutengeneza mazingira bora ya kuweza kupanda hadi Ligi Kuu.
Michezo Kuchochea Uchumi wa Mkoa
Mhandisi Jumbe pia amesisitiza umuhimu wa michezo katika kuchochea uchumi wa mkoa wa Shinyanga.
Amesema kuwa michezo inatoa fursa kwa wafanyabiashara, mama ntilie, na watoa huduma wengine kuongeza kipato kutokana na wingi wa mashabiki na watu wanaokuja kutazama mechi.
“Faida za michezo ni kubwa sana. Inachochea uchumi, inawasaidia wafanyabiashara, na inakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali. Hivyo, ni muhimu kuendelea kuhamasisha michezo katika mkoa wetu,” amesema.
Wito kwa Wachezaji na Wadau wa Michezo
Mhandisi Jumbe ametoa wito kwa wachezaji wa Stand United kuendelea kujituma zaidi uwanjani ili waweze kufikia malengo yao ya kupanda hadi Ligi Kuu.
Sehemu ya Wachezaji wa Stand United
Ameahidi kuwa hata kama timu itafunga magoli kumi, atayalipia, lakini amewataka wadau wengine wa michezo mkoani Shinyanga kuungana pamoja ili timu ya Stand United iweze kufikia mafanikio hayo.
Msaada wa Usajili wa Wachezaji
Mbali na motisha ya kifedha, Mhandisi Jumbe ameeleza kuwa atatoa ushirikiano wa kifedha katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo, ili Stand United iweze kuongeza wachezaji bora na kufanya vizuri zaidi katika michuano ya Ligi ya Championship.
Kwa upande wake, Meneja wa Timu ya Stand United, Meja Mingange, amemshukuru Mhandisi Jumbe kwa kujitolea na kutoa motisha kwa timu.
Amesema kuwa msaada huo utaongeza morali kwa wachezaji na uongozi kwa ujumla, na utasaidia sana timu kufanya vizuri zaidi katika michuano inayoshiriki.
Mhandisi James Jumbe ameonesha kwa vitendo jinsi wadau wa michezo wanavyoweza kuhamasisha maendeleo ya michezo katika mkoa wao.
Kwa msaada huu wa kifedha, timu ya Stand United ina nafasi nzuri ya kufanya vyema na kutimiza ndoto ya kurejea Ligi Kuu.
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza leo, Jumatatu Novemba 25, 2024, wakati akikabidhi jumla ya shilingi milioni 3.5 kwa timu ya Stand United inayoshiriki Ligi ya Championship, pamoja na shilingi milioni moja kama sehemu ya kununua magoli yaliyofungwa na timu hiyo katika michezo yake miwili ya hivi karibuni. Picha Malunde Media
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi fedha kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe akizungumza wakati akikabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 3.5 kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe (kushoto) akikabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 3.5 kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga ambapo ameahidi kutoa shilingi Milioni 3.5 kila mwezi kwa timu hiyo
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe (kushoto) akikabidhi shilingi Milioni 1 magoli matano yaliyofungwa kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga hivi karibuni, ambapo ameahidi kutoa shilingi 200,000/- kwa kila goli litakalofungwa na Stand United
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe (kushoto) akikabidhi shilingi Milioni 1 magoli matano yaliyofungwa kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga hivi karibuni, ambapo ameahidi kutoa shilingi 200,000/- kwa kila goli litakalofungwa na Stand United
Meneja wa Timu ya Stand United, Meja Mingange akitoa neno la shukrani wakati Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe fedha kwa Timu ya Stand United ya Mkoani Shinyanga
Mdau mkubwa wa michezo mkoani Shinyanga Mhandisi James Jumbe (wa pili kulia) akiwa na wadau wa michezo katika Uwanja wa CCM Kambarage
Mchezo kati ya Stand United na Mbeya City ukiendelea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Mchezo kati ya Stand United na Mbeya City ukiendelea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Mdau wa Michezo, Mhandisi Jumbe (katikati) akifuatilia mchezo kati ya Stand United na Mbeya City ukiendelea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Novemba 25,2024 Mchezo kati ya Stand United na Mbeya City ukiendelea katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga
No comments:
Post a Comment