Na Saida Issa, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa hadi sasa jumla ya dharura 2816 kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa pwani zimesafirishwa kwa kutumia mfumo wa m-mama.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa afya Dkt.Godwin Mollel alipouliza akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Subira Mgalu alipouliza Je, Serikali imejipangaje kuanzisha mpango wa m-mama katika visiwa vya Kibiti, Mafia na Mkuranga ili kupunguza vifo vya Akina Mama Wajawazito.
"Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Pwani ulianza kutumia mfumo wa M-Mama tarehe 15 Septemba 2023,
Mkoa huu umeingia mkataba na madereva ngazi ya jamii 112 ikihusisha madereva 14 toka Halmashauri za Kibiti na Mafia wanaotumia boti,"amesema.
Ameongeaza kuwa" Naomba kusema kuwa mfumo huu unafanya kazi katika maeneo yote ya nchi yetu hivyo nawaomba waheshimiwa wabunge wote kwanza kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya Namba 115 wawapo na dharura itokanayo na uzazi wakati wa ujauzito, kujifungua na hadi siku 42 baada ya kujifungua na kwa mtoto mchanga siku 0-28,"amesema.
No comments:
Post a Comment