BAJETI YA SERIKALI 2025/26 KUONGEZEKA KWA TRILIONI 5.72, SERIKALI YAKUSUDIA KUKUSANYA TRILIONI 55.06 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 1, 2024

BAJETI YA SERIKALI 2025/26 KUONGEZEKA KWA TRILIONI 5.72, SERIKALI YAKUSUDIA KUKUSANYA TRILIONI 55.06


Na Saida Issa, Dodoma 

MWENYEKITI wa kamati ya Bunge ya Bajeti Oran Njeza amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26

Serikali imekusudia kukusanya jumla ya Shilingi trilioni 55.06. 


Ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 11.58, la shilingi trilioni 5.72

ukilinganisha na Bajeti ya Mwaka ya Mwaka 2024/25 iliyokuwa na jumla ya shilingi trilioni 49.35


Hayo aliyaeleza Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati ya bajeti kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/26 pamoja na mapendekezo ya mwongozo wa maandaliazi ya mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/26. 


Akizungumza Mapato ya Ndani mwenyekiti huyo alisema uchambuzi wa Kamati umebaini kwamba mapato ya ndani yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Serikali za Mitaa,Maduhuli ya Wizara, Idara na Wakala pamoja na Mapato

ya Msajili wa Hazina yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 12.57 sawa na Shilingi trilioni 4.351. 


"Aidha, mikopo kwa ajili ya kudumisha deni la ndani (Roll over) malipo

yameshuka kwa asilimia 17.32 kutokana na kupungua kwa kiasi kinacholipwa (Redemption Profile) Jedwali Na.

10. Linaonyesha makadirio ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/26,


Uchambuzi wa Kamati umebaini

kwamba ukuaji wa uchumi unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 pamoja na mfumuko wa bei usiozidi asilimia 5

ni wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Serikali kufikia malengo ya makusanyo kwa asilimia 2 hadi 3

kulingana na mwenendo wa miaka iliyopita,"amesema.

No comments:

Post a Comment