MALEZI BORA NI MSINGI WA KUJENGA KIZAZI CHENYE MAADILI NA UZALENDO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 11, 2026

MALEZI BORA NI MSINGI WA KUJENGA KIZAZI CHENYE MAADILI NA UZALENDO


Na WMJJWM – ARUSHA


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju, amefungua kikao kazi cha siku tano kinacholenga kuandaa jumbe mahsusi za kuelimisha wazazi na walezi kuhusu malezi bora ya watoto na ustawi wa familia katika jamii. Kikao hicho kinafanyika kuanzia Machi 9 hadi 13, 2026 jijini Arusha.
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watoto, wanafunzi, wakufunzi, waandishi wa habari, wasanii, wataalamu wa afya pamoja na wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kushirikiana kuandaa benki ya jumbe zitakazotumiwa kuelimisha jamii kupitia vyombo mbalimbali vya Habari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mpanju amewataka washiriki kubuni jumbe zenye nguvu zitakazosaidia kuleta mabadiliko chanya hasa kwa watoto na vijana wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mmomonyoko wa maadili unaochangiwa na kuiga tamaduni za mataifa mengine kupitia maendeleo ya teknolojia

No comments:

Post a Comment