Dondoo za yaliyozungumzwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa na Katibu Mtendaji wa Chemba ya Migodi Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka katika Kipindi cha Asubuhi ya Jiji cha City Fm leo Novemba 15, 2024
DKT. STEVEN KIRUSWA, NAIBU WAZIRI WA MADINI:
1. Fursa za Uwekezaji kupitia Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Madini:
• Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unaongeza fursa kwa Tanzania kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
• Kupitia mkutano huu, Serikali inalenga kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha uwekezaji wa madini Afrika. Kuanzia hatua ya utafiti, uchimbaji, usafishaji au kuongezea thamani hadi kufika sokoni.
2. Dhima ya Mkutano 2024:
• Kaulimbiu: "Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii".
• Dhima hii inalenga kuimarisha mnyororo wa thamani wa madini, kuanzia utafiti, uchimbaji, uongezaji thamani, hadi kufikia masoko ya kimataifa.
3. Maendeleo ya Utafiti wa Madini:
• Hivi sasa, ni asilimia 16 tu ya eneo la nchi limefanyiwa utafiti wa kina wa madini.
• Kupitia mpango wa Vision 2030, serikali imelenga kuongeza kiwango cha utafiti wa madini hadi kufikia asilimia 50 ya eneo la nchi.
4. Nishati Safi na Madini Mkakati:
• Tanzania imejaaliwa kuwa na madini muhimu kwa wingi kama vile kinywe (graphite) nickel, cobalt, na lithium.
• Sheria zetu ziko wazi kwamba Mwekezaji yeyote ili apewe leseni ya kuchimba madini mkakati ni lazima atuonyeshe mpango wa kuyasafisha au kuyaongezea thamani hapa hapa nchini ili kulinda ajira za watanzania.
• Kama taifa tunaongeza juhudi Zaidi ili kuja kuwa moja kati ya wanchangiaji wakubwa wa nishati safi kwa kuhakikisha usimamizi bora wa madini mkakati
5. Mchango wa Wachimbaji Wadogo:
• Wachimbaji wadogo wanachangia asilimia 40 ya pato katika Sekta ya Madini.
• Serikali imeanzisha programu za kuwasaidia, ikiwemo Mining for Brighter Tomorrow (MBT) kwa lengo la kuwasaidia wachimabji wadogo hususan vinjana na wanawake sambamba na kuwafundishamMbinu bora za uchimbaji pamoja na kuwaunganisha na masoko ya uhakika kupitia Masoko ya Madini.
6. Uthamini wa Serikali kwa Wachimbaji Wadogo:
• Serikali inawathamini na kutambua mchango wa wachimbaji wadogo kwa kuhakikisha wanapata huduma stahiki bila usumbufu.
• Masoko ya madini yameimarishwa ili kudhibiti utoroshwaji wa madini na kuimarisha mapato ya Serikali, hadi sasa kuna jumla ya masoko 43 pamoja na vituo vuya ununuzi 105 nchi nzima.
• Serikali imesaidia kuongea na Taasisi na fedha na Mabenki na tayari benki kadhaa zimekubali kutoa mikopo kwa masharti nafuu kuliko hapo awali. Taasisi hizo pia zimeweza kuijua sekta vizuri na kuona kama fursa nyingine pia.
7. Kipaumbele kwa Wanawake katika Sekta ya Madini:
• Wanawake wanahimizwa kuunda vikundi na kumiliki leseni za uchimbaji. Tayari watu wetu wanaosimamia sekta mikoani wanashughulikia hilo sambamba na kuwashauri namna bora ya kuendesha shughuli zao.
• Serikali imeweka mikakati maalum ya kuwapa fursa zaidi wanawake kushiriki katika sekta hii ikiwemo kupitia MBT niliyoeleza kabla.
• Kupitia makundi yao wanaweza kupata mikopo kupitia ile mikopo ya asilimia 10 za halamshauri lakini pia kutoka benki pia.
8. Hamasa kwa Wazawa:
• Serikali inaendelea kuhamasisha Watanzania kuchangamkia fursa katika sekta ya madini, zikiwemo huduma za kiufundi, uwekezaji wa moja kwa moja, na utekelezaji wa Sera ya Ushiriki wa Watanzania katika mnyoro mzima wa shighuli za madini (Local Content).
……………………………………………………............…
ENG. BENJAMIN MCHWAMPAKA, KATIBU MTENDAJI WA CHEMBA YA MIGODI TANZANIA (TCM):
1. Nafasi ya Chemba ya Migodi Tanzania (TCM):
• Chemba ya Migodi Tanzania (TCM) ni shirikisho la wachimbaji wakubwa na wa kati katika sekta ya madini.
• TCM inashirikiana na serikali kuhakikisha sekta inakuwa kwa ufanisi na kwa njia endelevu.
2. Ushiriki wa TCM kwenye Mkutano:
• Mkutano huu ni jukwaa la kipekee kwa makampuni makubwa kufahamu na kuchangamkia fursa zilizopo katika sekta ya madini nchini Tanzania.
• TCM inahakikisha wanachama wake wanapata taarifa muhimu na kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa sera bora.
3. Kuimarisha Sekta kwa Kushirikiana na Serikali:
• TCM inatoa mchango mkubwa katika kuimarisha uwekezaji, kuhakikisha mazingira rafiki ya kibiashara, na kuhamasisha uongezaji thamani wa madini.
4. Kuimarisha Uhusiano wa Wadau:
• Chemba inafanya kazi ya kuunganisha Wachimbaji Wakubwa na wa Kati, kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano mzuri na kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi sambamba na ukuaji wa Sekta kwa ujumla
No comments:
Post a Comment