WAAMBIENI UKWELI USHIRIKI WA VYAMA VYAO KATIKA UCHAGUZI - MCHENGERWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 16, 2024

WAAMBIENI UKWELI USHIRIKI WA VYAMA VYAO KATIKA UCHAGUZI - MCHENGERWA




NA Okuly Julius _Dodoma


Serikali imewataka wadau wa uchaguzi, vikiwemo vyama vya siasa kuacha kufanya propaganda ambazo hazina ukweli na zinazoleta taharuki inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani, badala yake waendelee kueleza umma wa watanzania ukweli na uhalisia juu ya ushiriki wa vyama vyao katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 .

Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 16, 2024 kuhusu mchakato wa kuchukua, kurejesha, uteuzi pamoja na rufaa za wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema ukweli utawasaidia kujenga imani ya wananchi ili wawaamini na kukubali kugombea kupitia vyama vyao.

"Ni vyema kuwaambia ukweli wananchi kwani Ukweli huo utawasaidia kujenga imani ya wananchi ili wawaamini na kukubali kugombea kupitia vyama vyao," amesisitiza Mchengerwa

Aidha, Mchengerwa amesema kuwa takribani rufaa 16,309 zimepokelewa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili ambapo kati ya hizo rufaa 5,589 zimezokubaliwa.

Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefanikiwa kuweka wagombea katika nafasi zote za vijiji, vitongoji na mitaa huku upinzani ukiweka wagombea 30,977 sawa na 38% ya nafasi zote 80,430 zinazoshindaniwa.

Katika hatua nyingine
Mchengerwa amebainisha naafasi zitakazogombewa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 ni mwenyekiti wa kijiji nafasi 12,280, mwenyekiti wa mtaa nafasi 4,264, mwenyekiti wa kitongoji nafasi 63,886, wajumbe wa Serikali ya kijiji 230,834 pamoja na wajumbe wa kamati ya mtaa 21,320.

Nafasi zote zinazogombewa ni 80,430 (tukitoa nafasi za wajumbe wa Serikali za vijiji na kamati za Mitaa) ambazo zinajumuisha vijiji 12,280, mitaa 4,264 na vitongoji nafasi 63,886. Katika nafasi hizo zinazogombewa vyama 18 vya siasa ukiacha Chama cha Mapinduzi ambacho nimeshaeleza awali kimeweka wagombea katika nafasi zote, vyama hivyo vimeweza kuweka wagombea katika nafasi 30,977 kati ya nafasi 80,430 sawa na asilimia 38.51.



No comments:

Post a Comment