Na Ashrack Miraji, Same Kilimanjaro.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kihurio wilayani Same mkoani Kilimanjaro wameishukuru serikali kwa kuwapatia mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.17 ambayo itakuwa mwarobaini wa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi zaidi ya elfu 10,000 wa kta hiyo.
Pili Salim, ni miongoni mwao wakazi wa kata hiyo anasema kukamilika kwa mradi huo kutakuwa suluhisho juu ya adha wanayoipata ya kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji kwenye mito.
Kauli ya wananchi hao inaungwa mkono na katibu wa mbunge wa jimbo la Same Mashariki Semu Mmamba akisema huduma ya maji ni hitaji kubwa kwa wananchi wa Kihurio, akiombae mkandarasi kuanza utekelezaji wa mradi huo kama mkataba unavyomtaka.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo meneja wa Wwakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mha. Abdallah Gendaeka amesema kuwa mradi utatekelezwa kwa muda wa mika miwili kuanzia Desemba 6,2024 na kutarajiwa kukamilika Desemba 6,2026.
Kazi hiyo itafanya na mkandarasi kutoka kampuni ya FESAM CONSTRUCTION LIMITED yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam (mkandarasi mzawa).
Kwa upande wake Mhandisi Weransari Munisi, meneja wa RUWASA Mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa kupatikana kwa fedha za mradi huo kunachagizwa na jitihada za mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Mhe. Anne Kilango kwa lengo la kutaka wananchi wake kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba na kumtambulisha mkandarasi wa mradi huo, mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuhakikisha utekelezaji wa mradi unafyika kwa viwango vya utekelezaji wa miradi ya serikali kwa kuzingatia mkataba unavyomtaka ili kusaidia kuondoa adha ya upatikanaji wa maji kwawananchi wa kata ya Kihurio.
Aidha DC Kasilda amesisitiza pia wananchi wa Kihurio kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa mkandarasi kwenye kipindi chote cha utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamona na kila mmoja kuwa mlinzi wa kwanza wa mitambo itakayotumiwa na wakandarasi kutekeleza mradi huo.
“Namshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleza jitihada zake za dhati za kumtua mama ndoo kichwani, mradi huu unaenda kuwa mkombozi kwa Wananchi wangu wa kihurio ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiteseka na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji kwenye mito”. Alisema DC Kasilda.
Pia amempongeze mbunge wa jimbo la Same Mashariki mama Anne Kilango kwa namna ambavyo anawapambania wananchi wake kuhakikisha huduma mbalimbali za kijamii kwenye jimbo lake zinaimalika.
Naye Mha. Charles Maganga kutoka FESAM CONSTRUCTION LIMITED ameahidi kuifanya kazi hiyo kwa wakati kulingana na mkataba unavyomtaka ili mradi uweze kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na serikali.
No comments:
Post a Comment