Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali sa Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaelekeza wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi kuwasaidia wapiga kura kusoma orodha ya majina vizuri ili wote waliojiandikisha wapate fursa ya kupiga kura.
Mhe. Mchengerwa amesema hayo mara baada ya kupiga kura katika kituo chake alichojiandikishia cha Umwe Mchikichini kilichopo Ikwiriri Jimboni kwake Rufiji Mkoa wa Pwani, Waziri Mchengerwa amesema taarifa alizonazo mpaka sasa uchaguzi unaendelea kwa hali ya amani na utulivu nchi nzima.
No comments:
Post a Comment