WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KARAKANA YA TGFA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI KWA VIWANGO NA KWA WAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 29, 2024

WAZIRI SIMBACHAWENE AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA KARAKANA YA TGFA AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI KWA VIWANGO NA KWA WAKATI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Menejimenti ya Wakala ya Ndege za Serikali wakati wa kikao kazi chake na menejimenti hiyo kilicholenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (aliyenyoosha kidole) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam. Wengine ni Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitazama mchoro wa Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali Prof. Mhandisi Idrissa Mshoro wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali kilicholenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala hiyo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akielekea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtedaji Mkuu wa TGFA, Capt. Budodi Budodi (kulia) akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Menejimenti ya Wakala hiyo kilicholenga kukagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es Salaam.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemtaka Mkandarasi SUMA JKT anayejenga Karakana ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kukamilisha haraka ujenzi wa karakana hiyo na kwa viwango ili ianze kutumika kama ilivyokusudiwa.

Mhe. Simbachawene amesema hayo tarehe 28 Novemba, 2024 wakati wa kikao kazi chake na Menejimenti ya TGFA na Mkandarasi SUMA JKT mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa karakana hiyo jijini Dar es Salaam.

“Muongeze nguvu ili kazi ifanyike kwa haraka na kwa viwango kulingana na makubaliano yaliyofikiwa, mjitahidi kwa muda uliobakia, vinavyopaswa kukamilika vikamilike kwa wakati,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.

Aidha, ameisisitiza Menejimenti ya Wakala hiyo kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa haraka na kukamilika kwa wakati.

“Nitoe msisitizo kwa Menejimenti ya TGFA kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya ujenzi wa Karakana hii, binafsi nitajitahidi kufuatilia kwa karibu sana kwani tunahitaji ukamilike kwa wakati kama ilivyokusudiwa,” Mhe. Simbachawene ameongeza.

Akitoa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa kararakana hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TGFA, Capt. Budodi Budodi amesema, mradi wa Karakana ya Wakala ya Ndege za Serikali umeanza tarehe 7 Mei, 2023 na unarajiwa kukamilika tarehe 6 Mei, 2025.

No comments:

Post a Comment