BILIONI 1.5 ZAPATIKANA BAADA YA UUZAJI WA HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA SAMIA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 16, 2024

BILIONI 1.5 ZAPATIKANA BAADA YA UUZAJI WA HATIFUNGANI YA MIUNDOMBINU YA SAMIA DODOMA



Na Okuly Julius _ Dodoma


Kutokana na changamoto ya miundombinu ya barabara iliyopo nchini serikali ya Awamu ya sita imedhamiria kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuchochea maendeleo katika sekta mbalimbali.

Kauli hiyo ya serikali imekuja baada ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango NOVEMABA 29 2024 kuzindua Hatifungani ya miundombinu ya Samia ambapo mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amekusanya kiasi cha shilling bilioni 1.5 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika hafla ya uuzaji wa hati fungani ya miundombinu ya Samia mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani kutumia fursa ya hatifungani ya miundombinu ya Samia kwa kujenga barabara imara na zitakazokamilika kwa wakati ili kurahisisha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Kwa upande wake Vivian Komu Mwenyekiti wa Bodi wa Wakandarasi mkoani Dodoma amesema wao fedha hizo za hatifungani ya miundombinu ya Samia zitawasaidia wakandarasi kutekeleza majukumu yao ya miradi hasa wakati ambao serikali inakuwa haina fedha.

Hatifungani ya miundombinu ya Samia ni hati fungani mahsusi inayotolewa na benki ya CRDB kwa ajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) na Miradi hiyo itaongeza mtandao wa usafiri nchini, ikiboresha kwa kiasi kikubwa usafiri wa vijijini na mijini na Bondi hii inalenga kukusanya bilioni mia hamsini (150,000,000,000/=) na imepitiwa na kuidhinishwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CMSA.


No comments:

Post a Comment