WANANCHI WALIYOPO KARIBU NA MIRADI YA MAJI WANUFAIKE - NAIBU WAZIRI KUNDO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 16, 2024

WANANCHI WALIYOPO KARIBU NA MIRADI YA MAJI WANUFAIKE - NAIBU WAZIRI KUNDO




Na Okuly Julius _DODOMA


Serikali imeielekeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuhakikisha wananchi waliokaribu na miradi ya maji wananufaka na sio kuwa watazamaji wa miradi hiyo iliyopo katika maeneo yao bila kunufaika nayo.

Hayo yamesemwa leo Disemba 16,2024 na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi KUNDO MATHEW katika Ziara ya kukagua Miradi ya Maji ya Ujenzi wa Visima Pembezoni mwa Mji katika Jiji la Dodoma.

Amesema Serikali inategemea kufunga Prepaid Meter ili kupunguza malalamiko ya baadhi watu na taasisi kutolipa ankara za maji kwa wakati.
Pia ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maji kwa ufanisi.

Aidha, ameiagiza DUWASA kuweka utaratibu wa kuvuna maji ya mvua katika mradi wa Nzuguni, kwani maji yanayotiririka yamekuwa yakisababisha mmomonyoko wa udongo hivyo kuathiri baadhi ya miundombinu ya maji na kwamba suala la kuvuna maji ya mvua likifanyika litaleta matokeo makubwa.

Ametoa wito kwa watanzania kulinda vyanzo vya maji, miundominu ya maji na kutoa elimu kuhusu matumizi bora ya maji.

Mhe. Kundo amesema Serikali inatambua changamoto ya upatikanaji maji katika Jiji la Dodoma na kwamba imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na hali hiyo ikiwemo mipango ya muda mfupi, wa kati na kudumu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma Mhandisi Aron Joseph amemhakikishia Naibu Waziri wa Maji kutekeleza maagizo yote aliyotoa katika miradi ya maji Nzuguni, Kisasa Mwangaza na Nala Chihoni.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba amesema DUWASA inatekeleza miradi ya maji inayoonesha thamani halisi ya fedha.

Baadhi ya wakazi wa Chihoni Kata ya Nala, wakazi wa Kisasa pamoja na Diwani wa Kata ya Nala wameiomba DUWASA kuwaunganisha na huduma ya maji katika Kijiji chao kutokana na uwepo wa mradi wa usambazaji maji kwenye eneo lao.



No comments:

Post a Comment