DARAJA MTO UDAHAYA-KATA YA MASIEDA MKOMBOZI HALMASHAURI YA MBULU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 12, 2024

DARAJA MTO UDAHAYA-KATA YA MASIEDA MKOMBOZI HALMASHAURI YA MBULU



Na Mwandishi Wetu Mbulu, Manyara


Imeelezwa kwamba kukamilika kwa daraja la mto Udahaya pamoja na matengenezo ya barabara katika Kata ya Masiga linalounganisha Kata za Masieda, Gunyoda, Endahagichani, Maranga na Daudi, ambazo kata hizo zinaunganisha Mkoa wa Manyara na Kata ya Baray Mkoa wa Arusha na hivyo kuwasaidia wananchi katika shughuli zao za kusafirisha mazao.

Hayo yameelezwa na Diwani Kata ya Masieda Mhe. Nicomedy Nada wakati wa ukaguzi wa daraja hilo ambalo limekuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hizo hususan wanafunzi ambao huvuka mto huo kuelekea shuleni.

Amesema kukamilika kwa daraja hilo limekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi hao kwani wameondokana na adha ya kusombwa na maji hususan wakati wa masika ambapo watu wengi walikuwa wakipoteza maisha wakiwemo wanafunzi na watoa huduma ambao kila siku iliwapasa kuvuka upande wa pili.

‘Tunaishukuru Serikali kupitia TARURA kwa kutujengea daraja hili pamoja na kutuchongea barabara, hapo awali wanafunzi na watoa huduma walipokuwa wakivuka upande wa pili kufuata huduma za kijamii zikiwemo huduma za shule, ibada na hata huduma za afya walipoteza maisha, kuna mwaka muuguzi wa kituo cha afya, watoto na mifugo walichukuliwa na maji”.

“Daraja limekuwa na manufaa makubwa sana, linatusaidia kufanya biashara na shughuli zetu zingine, wananchi wamefurahi sana hatutashindwa kufanya kazi zetu sasa” Aliongeza.

Aidha, Mhe. Nada ameishukuru Serikali na Mbunge wao kwa kuwapigania na kuwapatia fedha na kusimamia ujenzi huo hadi kukamilika.

Naye, Bi. Rahel Severine mkazi wa Masieda amesema kwamba kabla ya daraja hilo walikuwa wakipata shida sana kwani korongo lilikuwa halipitiki hasa wakati wa mvua, ila kwa sasa wanashukuru kwani wanapita muda wote hata kama mto ukijaa maji imekuwa ni rahisi sana.

Ameongeza kusema kwa upande wa akina mama hata anapokaribia kujifungua imekuwa rahisi kupelekwa kwenye zahanati na kujifungua salama .


Pia Bw. Daniel Petro makazi wa kitongozi cha Udahaya ‘B’amesema daraja la Masieda limekuwa mkombozi kwao kwani awali lilishawasomba waumini sita waliokuwa wanatoka kanisani pia wanafunzi wa shule , hivyo kwa ujenzi wa daraja hilo wamekuwa wakipita mara kwa mara kwenda vitongoji vingine.

Wakati huo huo Mtendaji kata ya Masieda Bw. Athumani Govela amesema daraja hilo limewasaidia sana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwani awali wananchi walikuwa wakipata shida kutoka Masieda kwenda mjini hasa kipindi cha masika pia kumfuata mgonjwa wananchi walikuwa wakipata shida sana.

“Kabla ya ujenzi wa daraja hili utoro ulikithiri sana kwani wananfunzi walikosa masomo kwa kuwa hawakuweza kuvuka, lakini baada ya kujengwa kwa daraja hili limeweza kutusaidia sana, tumepoteza sana ndugu zetu”.

Hata hivyo amesema wanaendelea kutumia mikutano ya vijini na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kutumia njia za kwenye mabonde bali watumie daraja walilojengewa na kuahidi kuendelea kulitunza daraja hilo kwani limekuwa mkombozi katika kata zao na viongozi wa vitongoji wanahakikisha hakuna uharibifu wa miundombinu hiyo kwani Serikali imetumia gharama kubwa kulijenga.





No comments:

Post a Comment