DUWASA YAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI ENEO LA NKUHUNGU DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 4, 2024

DUWASA YAFANIKIWA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI ENEO LA NKUHUNGU DODOMA



Na Gideon Gregory, Dodoma.


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), imefanikiwa kutatua changamoto ya maji ambayo ilikuwa ikiwakumba wakazi wa Mtaa wa Bochela kata ya Nkuhungu kwa kuwachimbia kisima cha maji chenye urefu wa mita 170.

Baadhi ya wananchi wa mtaa huo wakizungumza leo Disemba 4,2024 mara mara baada ya kwenye ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya uchimbaji wa kisima hicho iliyofanywa na DUWASA wamesema hapo awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji jambo ambalo lilikuwa linakwamisha shughuli zao za kiuzalishaji.

"Kwanza tunaishukuru serikali pamoja na DUWASA kwa kuweza kuteletea kisima hiki kwani tumeteseka kwa muda mrefu kutafuta maji watoto wetu, wanawake na wanaume wote tumekuwa tukipata shida sana na ukijaribu kuona kwamba maji ndiyo uhai wa mwanadamu hivyo hatuna budi kuweza kulizumgumzia hili kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu,"wamesema.

Pia wameahidi kukitunza kisima hicho kwani ndiyo mkombozi wao na kuhakikisha kinakuwa salama muda wote na hakuna atakayekiharibu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Bochela Julius Ezekiel ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakitunza kisima hicho na kuondokana na taswira ya kuwa ni mali ya shule na wao hawausiki kwa jambo lolote.

"Haya maji ni kwaajili ya wananchi wote ambao wako katika mtaa huu Bochela na mitaa jirani, kwahiyo nitoe wito kwanza tutunze hivyo vyanzo vya maji na maji yenyewe kwani usipo yanywa utayaoga na maji ni muhimu sana,"amesema.

Aidha amewakumbusha wananchi kuwa Serikali ipo karibu nao, wametoka katika kuhangaika na maji nasasa uvumbuzi umepatikana na kuomba kuwa utatuzi huo usiishie Dodoma pekee uendelee na katika mikoa mingine hapa nchini.

Naye Mtafiti wa Maji chini ya Ardhi kutoka DUWASA Prince Isac amesema utekelezaji wa mradi huo wa kisima ni agizo kutoka kwa Waziri wa Maji katika ziara yake ya Kata ya Nkuhungu pamoja na Miganga ambapo aliagiza utafiti wa maji ufanyike ili wananchi waweze kupata maji.

"Kwasasa agizo hilo tumelitekeleza ambapo tumefanya utafiti wa maji na tumefanikiwa kupata sehemu nzuri eneo la hii Nkuhungu linalotoa maji na ndiyo kisima hiki tumefanikiwa kuchimba na maji tunapata,"amesema.

Amesema kwasasa kazi ya uchimbaji imekamilika ambapo kazi ilianza jana na leo mita 170 ziko tayari na hali ya maji iko vizuri hali inayofuata ni kwaajili ya uwekaji mabomba kisha baada ya hapo wakisafishe na mwisho wafanye zoezi la upimaji wingi wa maji ili kufahamu ndani ya saa kitakuwa kinatoa lita kiasi gani.






No comments:

Post a Comment