Maono ya Dkt. Samia Utalii Yazidi Kutekelezwa Mikumi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, December 10, 2024

Maono ya Dkt. Samia Utalii Yazidi Kutekelezwa Mikumi


Wakati akizindua filamu ya “Tanzania: The Royal Tour,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alitamani kuona mafanikio ya filamu hiyo yanaendelezwa kupitia miundombinu na huduma nyingine za utalii.

Hifadhi ya Taifa ya Mikumi imeendelea kutekeleza miradi ya mabilioni kujenga miundombinu ya kuanzia viwanja vya ndege, majengo ya kupokelea wageni na huduma za malazi.

Akitembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali hifadhini hapo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema sekta ya utalii nchini kwa sasa imekua kwa kasi kutokana na mikakati ya kutangaza utalii hivyo miundombinu hiyo itasaidia kuchagiza wageni zaidi kufika Mikumi.

“Kwa jiografia ya Mikumi hili ni eneo ambalo ndege nyingi zinatua hapa kutoka Zanzibar hivyo tunajenga uwanja mdogo lakini wa kisasa wa ndege, kuongeza malazi lakini tunakuja na mradi wa kujenga viwanja vya michezo na burudani ili watu wabarizi na kucheza ndani ya hifadhi huku wakiwaona wanyama huku na kule,” alisema Dkt. Abbasi.








No comments:

Post a Comment