TANROADS YAIMARISHA MATUMIZI YA HIFADHI YA BARABARA KANDA YA ZIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 14, 2024

TANROADS YAIMARISHA MATUMIZI YA HIFADHI YA BARABARA KANDA YA ZIWA


Mkurugenzi wa Matengenezo wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Dkt. Christina Kayoza, amegawa vifaa vya kupima umbali wa mkongo wa mawasiliano (OTDR) unaotumiwa na kampuni za simu ndani ya hifadhi ya barabara zinazohudumiwa na Tanroads .

Zoezi hilo limefanyika Mkoani Tabora kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Mohamed Besta, kwenye kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Vifaa hivyo vimetolewa kwa mameneja wa Tanroads mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma na Mara ili kuwasaidia katika upimaji wa umbali kwenye mkongo wa mawasiliano kwenye hifadhi ya barabara.

Uwepo wa vifaa hivyo, umeelezwa kwamba utaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa watumiaji wa hifadhi ya barabara hususani mikongo ya simu.

No comments:

Post a Comment