Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ambapo atafungua Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), leo tarehe 06 Disemba, 2024
Kongamano hilo limelenga kuwakutanisha Wahandisi na Mafundi Sanifu kutoka Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi kwa lengo la kujifunza, kujadili, kutathimini na kubadilishana uzoefu kuhusu shughuli zao za kihandisi.
No comments:
Post a Comment