
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amemtaka Mkandarasi Estim anaejenga barabara ya Mtanana-Kibaigwa Km 6, kuongeza kasi ili ikamilike kwa wakati.
Mradi huo unaohusisha ujenzi wa makalvati makubwa na uwekaji wa taa za barabarani umefikia asilimia 48.9 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 26 zitatumika.
"Meneja eneo hili limekuwa changamoto kwa muda mrefu hivyo simamieni kazi hii ifanyike kwa ubora tena usiku na mchana", amesisitiza Waziri Ulega.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma Eng. Zuhura Amani amesema Mkandarasi yupo ndani ya muda na ujenzi unaendelea vizuri hivyo amemhakikishia Waziri kusimamia kazi hiyo kikamilifu ili ikamilike kwa wakati na ubora uliokusudiwa.
Ujenzi huo ni sehemu ya mkakati wa Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja na kuweka taa ili yapitike wakati wote wa mwaka kwa usalama na kuchochea biashara katika maeneo ya miji.







No comments:
Post a Comment