
Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, ameanza ziara ya siku moja mkoani Mwanza leo Januari 24, 2025 ambapo pamoja na mambo mengine atakagua miundombinu ya Vivuko, Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo - Busisi) na barabara unganishi na kuzungumza na wananchi.
Waziri Ulega amepokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.




No comments:
Post a Comment