BMT: VILABU VYA LIGI KUU VIZURI KUWA NA VIWANJA VYAO BINAFSI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 18, 2025

BMT: VILABU VYA LIGI KUU VIZURI KUWA NA VIWANJA VYAO BINAFSI




Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amesema wana mpango wa kuja kutoa mwongozo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu nchini kuhakikisha wanakuwa na viwanja vyao binafsi vya michezo.

"Tunapoelekea tutatoa muda kwa vilabu vyote nchini vinavyoshiriki ligi kuu wawe na viwanja vyao vya michezo, kwahiyo tutawapa muda wa matazamio na kukaa nao kama mdau na kuzungumza nao juu ya hilo" alisema.

Neema ameyasema hayo leo Februari 18,2025 katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Baraza hilo kwa miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kuwa,Serikali ya Awamu ya Sita imeiongezea Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bajeti kutoka shilingi bilioni 35.44 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi shilingi bilioni 258 mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo bajeti hiyo imeirahisishia wizara na taasisi zake kutekeleza majukumu yake.

"Katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya michezo, Rais Samia amefanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa takriban shilingi Bilioni 31, ameanza ujenzi wa uwanja wa michezo Arusha utakaogharimu shilingi Bilioni 338 na Dodoma kwa shilingi Bilioni 310. Pia, anajenga viwanja vya mazoezi kwa gharama ya shilingi Bilioni 24" alisema Neema.

Kwa upande mwingine, Neema amesema BMT imefanikiwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya michezo ya Kimataifa, kuondoa kodi kwa nyasi bandia, Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya Tano na kuanzishwa kwa Mfuko wa Michezo.

Kwa upande mwingine, Msitha amesema wana mpango wa kutoa mafunzo kwa makocha katika michezo mbalimbali hapa nchini, kwa mwaka jana 2024 wametoa mafunzo kwa makocha kadhaa wa kimataifa katika mchezo wa ngumi.

No comments:

Post a Comment