KATIBU MKUU NISHATI AIPONGEZA SWEDEN KUFADHILI MIRADI YA UMEME NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 28, 2025

KATIBU MKUU NISHATI AIPONGEZA SWEDEN KUFADHILI MIRADI YA UMEME NCHINI


Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha.Felchesmi Mramba akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa jijini Dodoma wakati wa hafla ya kufunga rasmi Mradi wa Njia ya kusafirisha Umeme kutoka
Makambako hadi Songea, uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden na Tanzania.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Charlotta Ozaki Macias
akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma wakati wa hafla ya kufunga rasmi Mradi wa Njia ya kusafirisha Umeme kutoka Makambako hadi Songea, uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mha.Gissima Nyamo-Hanga akizungumza jambo wakati wa hafla ya kufunga rasmi Mradi wa Njia ya kusafirisha Umeme kutoka Makambako hadi Songea
uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.


🎈🎈Yakabidhi Mradi wa umeme wa Makambako-Songea

🎈🎈Ufadhili wake Mradi wa Makambako- Songea wawezesha vijiji 120 kupata umeme

🎈🎈Ni nchi ya kwanza kufadhili miradi ya umeme vijijini nchini

🎈🎈Balozi wa Sweden nchini atoa pongezi kwa TANESCO na REA usimamizi wa
miradi ya umeme

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba ameipongeza
Serikali ya Sweden kwa kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika
utekelezaji wa miradi ya umeme ikiwa ni pamoja na mradi wa Makambako
hadi Songea.

Pongezi hizo zimetolewa Februari 27, 2025 jijini Dodoma wakati wa
hafla ya kufunga rasmi Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme kutoka Makambako hadi Songea, uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Mhandisi Mramba amesema kuwa mradi huo wa njia ya umeme kutoka
Makambako hadi Songea umehusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme
yenye msongo wa kilovoti 220 kwa urefu wa kilomita 245, ujenzi wa vituo vya umeme vya Madaba na Songea mjini, upanuzi wa kituo cha umeme
cha Makambako pamoja na kusambaza umeme katika vijiji 120.

“Tunaipongeza Serikali ya Sweden kwa mchango mkubwa ambao wanatusaidia
katika kufadhili miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo kupeleka umeme
vijijini hapa nchini.” Amesema Mramba

Amesema kuwa, Serikali ya Sweden imetoa mchango mkubwa katika
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini iliyotekelezwa katika maeneo
mbalimbali ikiwemo Wilaya za Urambo, Serengeti, Simanjiro na Ukerewe,
pia Sweden ndio nchi ya kwanza kusaidia miradi ya umeme vijijini hapa
nchini.

Miradi mingine iliyofadhiliwa na Sweden ni mradi wa ujenzi wa Bwawa la
Mtera na Kidatu.

Ameongeza kuwa, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Sweden kwa
sasa inaendeleza ukarabati wa kituo cha kuzalisha umeme cha Hale
ambacho ni cha muda mrefu ambacho kitazalisha megawati 21 baada ya
ukarabati kukamilika.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias
ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la umeme Tanzania
(TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kusimamia kikamilifu
utekelezaji wa miradi ya umeme.

Amesema mradi wa Makambako hadi Songea uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka 20 kukamilika kwake kutaendelea kunufaisha wananchi wengi katika upatikanaji wa huduma ya umeme hasa maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment