RAIS MUSEVENI AWASILI TANZANIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 8, 2025

RAIS MUSEVENI AWASILI TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amewasili nchini Tanzania na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo tarehe 08 Februari 2025 

Rais Museveni atashiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika leo.

Jumuiya zote mbili zinakutana kwa pamoja kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment