RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UBUNIFU KATIKA SAYANSI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 11, 2025

RIDHIWANI KIKWETE AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UBUNIFU KATIKA SAYANSI



Na Okuly Julius _DODOMA


Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu kuliangalia eneo la Ushindani uliopo na utekelezaji wa Sera mpya ya Elimu ujikite katika kutatua changamoto zilizopo nchini.

Ridhiwani ameyasema hayo leo alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Na Wasichana katika Sayansi maadhimisho yaliyofanyika jijini Dodoma.

Amesema Serikali inaendelea kutambua changamoto ya Usonji katika jamii yetu, na katika kufanya hilo kupitia Sera Mpya ya Elimu, vijana wenye changamoto ya Usonji ambao ndani yao wana kipaji maalum nalo pia limeangaliwa.
.
"Tunacho chuo cha Patandi ambacho chuo hicho kinaendelea kuwaangalia na kuwafundisha walimu na kukuza vipaji Vya Vijana wenye Usonji, hivyo jambo hilo halijaachwa nyuma" alisema Waziri Ridhiwani.

Aidha amesema, kundi la Wanawake na Wasichana ni kundi ambalo linatengeneza asilimia 49.7 ya watu wote duniani, kwa mujibu Wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Tanzania, ambapo Wanawake na Wasichana ni Asilimia 51.3.

"Kiwango Cha Wanawake na Wasichana wanaoshiriki kwenye nyanja za kazi za STEM duniani zinakadiriwa kuwa Asilimia 33 pekee" alisema.

Aidha, Ridhiwani amesema tunapowawezesha Wasichana na Wanawake katika kushiriki Katika Sayansi na Uongozi, Sio tu tutaimarisha Usawa wa Kijinsia bali pia tutazidi kuimarisha utafiti ubunifu unaojibu changamoto na mahitaji ya kiuchumi na kijamii nchini na kwingineko.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni na Michezo Musa Ramadhani Sima amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita ni kuwafanya vijana wawe na ujuzi.

"kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya sita ni kuwafanya vijana wawe na ujuzi, kutengeneza elimu ujuzi na sisi Bungeni tumekuwa mstari wa mbele kuitaka Serikali vijana wetu wawe na ujuzi na hivi tunavyozungumza tayari wameshaanzisha shule la Amali, "amesema Sima

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dakta Charles Mahera amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023 na Mitaala Iliyoboreshwa imeweka msisitizo katika matumizi ya TEHAMA katika Kujifunzia na kufundishia.

"Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekamilisha Mkakati wa kitaifa wa matumizi ya TEHAMA ya kiteknolojia na kidijiti na miongozo ya namna mbalimbali ya kutumia Teknolojia hizo na miongozo ya kutumia Akili Unde kwa hivyo ninayo imani kuwa ushirikiano kati ya Serikali na wadau utasaidia kuongeza matumizi ya teknolojia Maradufu, "ameeleza Dkt. Mahera

Nao Baadhi ya wanafunzi wa Kike walioshiriki maadhimisho hayo wameelezea baadhi ya bunifu zao ambazo wamezitengeneza na furaha yao ya kusoma masomo ya Sayansi.













No comments:

Post a Comment