BUWSSA YAPITISHIWA MIRADI YA BILIONI 28.1 KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA DKT. SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 6, 2025

BUWSSA YAPITISHIWA MIRADI YA BILIONI 28.1 KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA DKT. SAMIA




Na Okuly Julius _DODOMA


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Bunda ( BUWSSA) Bi. Esther Gilyoma amesema tangu serikali ya awamu ya sita kuanza Mamlaka hiyo imepitishiwa miradi ya thamani ya TShs Bilioni 28. 18 ambapo kiasi cha Tshs Bilioni 11.894 tayari zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji wake unaendelea.

Ameaeleza hayo wakati akizungumuza na waandishi wa habari jijini hapa Dodoma Machi 6, 2025 juu ya mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita ambapo amesema kuwa tayari wamekwisha zifikia kata 12 na mbili zinaendelea kupatiwa huduma.

Amesema BUWSSA itahakikisha huduma ya maji inaendelea kuimarika katika mji wa Bunda kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo wanampango wa ujenzi wa tenki kubwa la maji kwenye mwinuko wa mita 1537 mlima Nyiendo wenye uwezo wa kubeba lita 5,000,000 ili kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji pindi umeme unapo katika.

"Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji wa Bunda hutoa huduma ya maji kwa wakazi wa mji wa Bunda na viunga vyake; hii inajumuisha vijiji vya Nyabehu, Guta, Tairo na Migungani; vijiji ambavyo bomba kuu linapita kupeleka maji mjini Bunda.Katika eneo la kiutendaji la Mamlaka ina jumla ya kata kumi na nne (14) ambapo kata kumi (12) zina huduma ya maji ya bomba kutoka ziwa Victoria, ambazo ni Bunda Mjini,Sazira,Nyatwari,Kunzugu,Guta,Kabasa,Balili,Nyamakokoto,Nyasura,Manyamanyama,Kabarimu na Bunda Stoo Kata mbili (2) zinapata huduma ya maji kupitia visima virefu,visima vifupi,vyanzo vya asili na kuna miradi ya maji kata ya Wariku na Mcharo inaendelea ili kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata majisafi na salama.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa eneo linalohudumiwa na Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingiraMji wa Bunda una wakazi 195,848 (2024) kati ya hao asilimia 85 % ambayo ni sawa na wakazi 165,613 ndio wanapata huduma ya maji ya bomba hivi sasa.

"Tangu awamu ya sita kuanza Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imepitishiwa miradi ya thamani ya TShs 28,180,572,033.71 na Tshs 11,894,976,776.81 taryari zimepokelewa na baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea",amesema.

Pia ameseama maji hayo huzalishwa kutoka Chanzo cha maji cha Nyabehu ambacho kipo umbali wa kilomita 24.8 kutoka mjini Bunda katika kijiji cha Nyabehu huku akieleza kuwa chanzo hicho kinachukua maji kutoka ziwa Victoria.

Amesema kipindi cha Mwaka 2021 maji yaliyokuwa yanazalishwa ilikuwa wastani wa meta za ujazo 2,976 m3 kwa siku ambapo kwasasa Maji yanayozalishwa ni wastani wa Meta za ujazo 5,160m3 na kwa siku uwezo wa uzalishaji unaweza kufikia 14,784 kutokana na usanifu uliofanyika na uzalishaji huo wa maji unaendelea kuongezeka siku kwa siku kutokana na mahitaji na upanuzi wa Mtandao wa bomba unaondelea kufanyika katika maeneo ya Wariku na Kisangwa.

"Upotevu wa maji kwa mwaka 2021 ulikuwa watani wa asilimia 64 kutokana na mtandao wa bomba chakavu uliojengwa kuanzia mwaka 1972, baada ya jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya sita (6) za kutoa fedha za kubadili bomba chakavu na mita goigoi upotevu wa maji kwa sasa ni asilimia 32 na unaendelea kushuka kutokana na jitihada zinazoendelea kufanyika"amesema.

Aidha amesema kwa mwaka 2021 Mamlaka ilikuwa inatoa huduma ya maji kwa wastani wa masaa 12 kutokana na ufinyu wa mtandao na kutokuwa na maji ya kutosha,kwa mwaka 2023 baada ya mradi mkubwawa kusafisha na kutibu maji Nyabehu Bunda kukamilika.

"Kwa sasa Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda inatoa huduma ya majisafi kwa wastani wa masaa 22 bila ya kuwa na mgawo wa maji, baada ya miradi miwili kukamilika ambayo kwa sasa inaendelea mradi wa kusambaza maji Wariku na mradi wa maji Kisangwa Mamlaka itatoa huduma ya maji kwa masaa 24 na kufikisha wastani wa utoaji wa huduma kwa wastani wa asilimia 96 na kufikia lengo la ILANI ya chama cha mapinduzi (CCM)",amesema.

No comments:

Post a Comment