TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 7, 2026

TANZANIA NA NORWAY KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadiliana namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akimkabidhi zawadi ya baadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadiliana namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akimkabidhi zawadi ya Saa yenye taswira yake, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes yenye picha yake, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadiliana namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, kati ya nchi hizo mbili.

(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)


Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Tanzania na Norway zinajivunia uhusiano imara wa kiuchumi, kijamii na kidiplomasia, uliochangia maendeleo ya nchi katika nyanja mbalimbali.

Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, wamejadiliana namna ya kuimarisha zaidi ushirikiano huo.

Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa Tanzania na Norway Mwaka 1964, nchi hiyo imekuwa mdau mkubwa katika kufadhili miradi ya kiuchumi na kijamii katika sekta za nishati, mafuta na gesi, usimamizi wa fedha za umma, kilimo, afya, elimu, mazingira, na kusaidia kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.

Mhe’s Balozi Omar alisema kuwa Serikali inatambua na kuthamini msaada wa ruzuku wa NOK 525 milioni (takriban TZS 136.5 bilioni) uliotolewa na nchi hiyo tangu 2020 kwa ajili ya kuziwezesha kaya masikini kiuchumi kupitia Program ya TASAF.

Alitumia fursa ya kikao hicho kuialika jumuiya ya wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Norway kuja kuwekeza nchi katika sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo.

Kwa upande wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes alipongeza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea nchini na kuahidi kuwa Norway itaendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa faida ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Alisema kuwa anatamani kuona kiwango cha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili kionangezeka zaidi kuliko kilivyo hivi sasa na kwamba ataendelea kuwashawishi wawekezaji wengi kutoka Norway kuja Tanzania kuwekeza.

Aidha, Mhe. Tinnes alisema kuwa Norway iko tayari kushirikiana na Tanzania kuwekeza katika sekta ya nishati na hifadhi ya mazingira hususan biashara ya hewa ukaa ambayo alisema ina fedha nyingi lakini pia ni muhimu kwa utunzaji mazingira.

No comments:

Post a Comment