Bwawa la Uyui kunufaisha wananchi zaidi ya elfu 90 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 14, 2025

Bwawa la Uyui kunufaisha wananchi zaidi ya elfu 90


Bwawa la Uyui linalojengwa kwa fedha za ndani kiasi cha Shilingi bilioni nne linatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi elfu 90.

Bwawa hilo
 linauwezo wa kuhifadhi kiasi cha maji lita bilioni 5.1 kwa mwaka.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo katika ukaguzi amepongeza na kuridhishwa na utekelezaji wa kazi hiyo ambayo imefika asilimia 60.

Ujenzi huo unafanyika katika kijiji cha Kizengi , Uyui.

Kamati hiyo imetoa shukran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mitambo ya kisasa ya uchimbaji wa mabwawa seti tano ili kufanikisha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.

Pamoja na hilo, kamati imempongeza Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) na wataalamu wa Sekta ya Maji kwa kazi ya kufikisha huduma ya majisafi kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment