DKT. MUYUNGI ASISITIZA KASI UJENZI WA JENGO LA OMR, MTUMBA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 10, 2026

DKT. MUYUNGI ASISITIZA KASI UJENZI WA JENGO LA OMR, MTUMBA DODOMA


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akipata maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma kutoka kwa Mratibu wa Mradi kutoka Kampuni ya Suma JKT, Mhandisi Richard Raphael (wa pili kulia). Ziara hiyo imefanyika Machi 9, 2026 Mtumba Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma Machi 9, 2026. Kushoto ni Mratibu wa Mradi kutoka Kampuni ya Suma JKT, Mhandisi Richard Raphael.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi akitazama samani mbalimbali zilizopo ndani ya mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa jengo hilo Machi 9, 2026. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Paul Masanja.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akizungumza jambo kwa Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo kutoka Kampuni ya Suma JKT, Mhandisi Richard Raphael wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo Machi 9, 2026. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Mhe. Balozi Baraka Luvanda.

Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohamed Salum (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Richard Muyungi wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma Machi 9, 2026.

Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohamed Salum (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Richard Muyungi wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma Machi 9, 2026. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ziara yake ya kujionea hatua iliyofikiwa katika mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma Machi 9, 2026. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Suma JKT kuongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Dkt. Muyungi amesema hayo Machi 09, 2026 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo ambapo aliongozana na Viongozi na Menejimenti kwa ajili ya kujionea na hatua iliyofikiwa katika mradi huo.

Amesema mkandarasi wa kampuni ya Suma JKT hana budi kufanya kazi masaa 24 ili kuwezesha maboresho na ukarabati wa baadhi ya maeneo ndani ya jengo ambayo hayajakamilika.

Ameongeza kuwa Ofisi yake haitongeza muda wa kukamilisha mradi huo kwa kuwa ilishafanya hivyo hapo awali na hivyo kumtaka mkandarasi hukakikisha anatumia vyema muda uliopo kuweza kukamilisha na kukabidhi jengo hilo.

Kamati ya Bunge inatarajia kufanya ziara katika mradi wa jengo hili tarehe 18 Machi mwaka huu, hivyo nawasisitiza kuhakikisha mnakamilisha kazi hii kwa wakati kabla ya tarehe hiyo kufika amesema Dkt. Muyungi.

Aidha Dkt. Muyungi amesema Ofisi yake imetimiza mahitaji yote yaliyohitajika kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo hilo ikiwemo malipo ya fedha kwa mkandarasi na ununuzi wa samani mbalimbali.

Pia Dkt. Muyungi amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anajenga miundombinu yenye mifumo ya kisasa ya uchakataji na usimamizi wa taka ngumu kuweza kutumia katika jengo hilo pindi litakapokamilika hatua inayolenga kutunza mazingira.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi kutoka Kampuni ya Suma JKT, Mhandisi Richard Raphael amesema kampuni itazingatia maelekezo yaliyotolewa na kuyafanyia kazi ili kuhakikisha mradi wa ujenzi wa jengo hilo unakamilika katika muda uliopangwa.

Katika ziara hiyo Dkt. Muyungi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda pamoja na menejementi ya ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment