COSOTA YATATUA MIGOGORO 118 YA HAKIMILIKI KATI YA 136 ILIYORIPOTIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 21, 2025

COSOTA YATATUA MIGOGORO 118 YA HAKIMILIKI KATI YA 136 ILIYORIPOTIWA


Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Haki Miliki Tanzania Bi. Doreen Sinare akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 21,2025 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika ofisi ya hakimiliki Tanzania (COSOTA)

 

Na Okuly Julius _ DODOMA

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Haki Miliki Tanzania Bi. Doreen Sinare amesema katika kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Ofisi hiyo imepokea jumla ya Migogoro 136.

Ameyasema hayo leo Machi 21,2025 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita chini ya mheshimiwa Dky. Samia Suluhu Hassan, katika ofisi ya hakimiliki Tanzania (COSOTA)

Amesema Kati ya Migogoro hiyo Migogoro 118 imetatuliwa, migogoro 10 haijafanyiwa kazi bado na Migogoro 8 bado inafanyiwa kazi.

"Mafanikio haya yanatokana na juhudi kubwa za serikali za kuhakikisha kuwa haki za wabunifu na wasanii zinalindwa ipasavyo,"

Na kuongeza kuwa “Lengo letu ni kuona kila mbunifu na msanii anapata stahili zake kwa mujibu wa sheria, na ndio maana tumejikita katika kushughulikia migogoro kwa ufanisi,” ameeleza Sinare

Pamoja na kushughulikia migogoro, COSOTA pia imekuwa ikihusika katika kesi kumi za hakimiliki, ikiwa ni hatua muhimu katika kulinda haki za wabunifu dhidi ya uharamia na matumizi yasiyoidhinishwa ya kazi zao.

Katika hatua nyingine Bi. Sinare amesema kupitia Tozo ya Hakimiliki , COSOTA imekusanya jumla ya shilingi bilioni 1.42 kuanzia Septemba, 2023 hadi Februari, 2025 ambapo Ofisi imefanikiwa kupokea fedha za tozo ya hakimiliki za mwaka wa fedha 2023/2024 kutoka Wizara ya Fedha zaidi ya shilingi milioni 840.

Kwa mujibu wa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki pamoja na Mabadiliko Sheria ya Fedha Na. 5 ya mwaka 2022, kiasi cha tozo ya Hakimiliki kilichokusanywa ndani ya mwaka husika hugawanywa kwa makundi manne katika asilimia.

Ambapo COSOTA inachukua 20%, Mfuko wa Utamaduni 10%, Mfuko Mkuu wa Serikali 10%, na Kampuni za kukusanya na kugawa mirabaha (CMOs) kwa ajili ya wasanii, waandishi na wamiliki wengine wa hakimiliki 60%.

Bi. Sinare amesema, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, usajili wa kazi zinazolindwa na Sheria ya hakimiliki na hakishiriki umeongezeka kwa asilimia 70 Ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kuanzia mwaka 2021 mpaka Februari 2025, COSOTA, imesajili kazi za Sanaa na uandishi 11,519 na Wabunifu 3,436.

" Idadi hii ya wabunifu pamoja na kazi zao imetokana na zoezi la utoaji wa elimu na mafunzo mbalimbali ya hakimiliki na usajili kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, semina lakini pia kushiriki matukio mbalimbali ya wadau ambapo COSOTA ilipata fursa ya kuelimisha wadau kuhusiana na hakimiliki na uhamasishaji wa usajili wa kazi za hakimiliki,"amesema

Na kuongeza" katika kipindi hicho kamati maalumu ya Usajili ndani ya COSOTA inayojihusisha na masuala ya usajili, imefanikiwa kutoa mafunzo na ufafanuzi kuhusiana na hakimiliki kwenye kazi zilizopokelewa katika kipindi hicho kwa idadi ya wabunifu 167, "ameongoza Sinare

Vilevile, katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu sita COSOTA imetoa jumla ya vyeti 7,679 vya uthibitisho wa umiliki wa hakimiliki kwa wabunifu waliosajili kazi zao.

Aidha, kwa mwaka 2021 - 2025 COSOTA imefanikiwa kufanya migao miwili kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipolihutubia bunge mwaka 2021 ambapo alisisitiza katika kipindi cha uongozi wake, serikali itahakikisha wabunifu wote wananufaika zaidi na kazi zao.

Ambapo Mgao wa kwanza ambao ulikuwa ni mgao wa ishirini na tatu ulifanyika tarehe 28/01/2022 na ulikuwa wa kiasi cha Tshs. Tshs. 312,290,259,000, ambapo Wasani 1,123 walinufaika, na ulitokana na matumizi ya kazi 5,924 za muziki ambazo zilitumika katika vituo 11 vya redio, ikiwemo redio katika ngazi ya kitaifa, Mkoa, wilaya, kijamii na za kidini.

Mgao wa pili katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita ulifanyika tarehe 21/07/2023 na ulikuwa ni mgao wa ishirini na nne wa mirabaha kwa kazi za muziki na COSOTA iligawa kiasi cha Tshs. 396,947,743.20 na wasanii wa muziki 8,165 walinufaika kupitia kazi zao 61,490.


No comments:

Post a Comment