Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Ujumbe kutoka Huawei Tanzania, ukiongozwa na Bw. Ross Chen, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Kanda ya Afrika Mashariki, umekutana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kujadili ushirikiano katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika sekta ya elimu.
Katika kikao hicho, kilichoongozwa na Prof. Daniel Mushi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi ya kidijitali inayolenga kuwezesha ufundishaji kwa kutumia TEHAMA.
No comments:
Post a Comment