Kamati ya Maji na Mazingira Yapongeza Ubora wa Mradi wa Maji wa Munanila - Nyakimue - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 16, 2025

Kamati ya Maji na Mazingira Yapongeza Ubora wa Mradi wa Maji wa Munanila - Nyakimue


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imepongeza utekelezaji wa kiwango katika mradi wa maji wa Munanila - Nyakimue ambao unanufaisha vijiji nane mkoani Kigoma.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) ametoa pongezi hizo mkoani Kigoma baada ya Kamati anayoiongoza kutembelea na kukagua mradi wa maji wa Munanila-Nyakimue.

Mhe. Kiswaga (Mb) amesema wamethibisha kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Maji katika ujenzi wa mradi huo ambao utaongeza kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini lengo likiwa kufika asilimia 85.

 
Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo Msimamizi wa Mradi Mhandisi Golden Katoto amesema kazi zilizofanyika ni pamoja na ununuzi na ulazaji wa bomba,Ujenzi wa nyumba za mitambo tatu ambazo zipo katika hatua za umaliziaji na ujenzi wa vituo vya umma vinne vya kuchota maji, ambapo vituo viwili vinatoa huduma.


Kamati ya Maji na Mazingira imesisitiza umuhimu wa suala la utunzaji wa miundombinu ya maji na kuhakikisha maji yanayozalishwa na miradi yanasambazwa kwa wananchi.


Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) akiongea kwa niaba ya Waziri wa Maji amesema Wizara ya Maji inaendelea na jitihada katika kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi wote.

 Mradi wa Maji wa Munanila-Nyakimue unathamani ya shilingi Bilioni 14.9 na utekelezaji umefika asilimia 67 ukitarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2025.

No comments:

Post a Comment