MABADILIKO YA KANUNI ZA UDAHILI VYUO VYA ELIMU YA KATI KULENGA KUBORESHA UBORA WA WAHITIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 28, 2025

MABADILIKO YA KANUNI ZA UDAHILI VYUO VYA ELIMU YA KATI KULENGA KUBORESHA UBORA WA WAHITIMU




Na Okuly Julius _ DODOMA


Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Jofrey Oleke, amesema kuwa mabadiliko ya kanuni za udahili wa vyuo vya elimu ya kati nchini yatasaidia kuhakikisha vyuo vinapata wahitimu bora watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Dkt. Oleke ameyasema hayo wakati akimwakilisha Katibu Mtendaji wa NACTVET Dkt. Mwajuma Lingwanda , katika ufunguzi wa Warsha ya Wadau kuhusu kupitia Kanuni za Udahili Vyuo vya Elimu ya Kati, iliyofanyika jijini Dodoma leo, Machi 28, 2025.

Amesema lengo kuu la warsha hiyo ni kupata maoni ya wadau kabla ya kanuni mpya kuanza kutumika.

"Ikumbukwe kwamba kanuni hizi zimehuwishwa kutokana na mabadiliko mbalimbali yaliyotokea, hasa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014, Toleo la 2023, ambayo imezinduliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni," alisema Dkt. Oleke.

Ameongeza kuwa mabadiliko hayo yanahakikisha kanuni hizo zinaendana na sera husika na mabadiliko ya taasisi, kwani awali NACTVET ilikuwa ikijulikana kama NACTE.

Aidha, Dkt. Oleke amesema kuwa manufaa makubwa ya kanuni hizo ni kuhakikisha kunakuwepo miongozo bora zaidi ambayo itaboresha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini.


Kwa upande wake, Katibu wa Umoja wa Wakuu wa Vyuo Tanzania, Mwl. Rashid Nditi, amesema kuwa warsha hiyo inalenga kukumbushana kuhusu taratibu na kanuni za udahili ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa mzuri.



No comments:

Post a Comment