TIB YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 630.3 KATIKA MIRADI YA MAENDELEO, YAZALISHA AJIRA 12,547 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 20, 2025

TIB YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 630.3 KATIKA MIRADI YA MAENDELEO, YAZALISHA AJIRA 12,547


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bi. Lilian Mbassy akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.




Na Okuly Julius DODOMA



Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Benki ya Maendeleo TIB imesema imefanikiwa kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 630.3 katika miradi ya maendeleo hadi kufikia Desemba 2024.

Kati ya kiasi hicho, Shilingi bilioni 408.3 zipo kwenye mizania ya Benki, huku mifuko tisa inayosimamiwa na Benki ikichangia uwekezaji
wa Shilingi bilioni 222, uwekezaji huo ni wa miradi ya muda wa miaka 5-15 katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Hayo yameelezwa Machi 20, 2025 Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bibi Lilian Mbassy, wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Taasisi hiyo.

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Bibi Mbassy amesema kuwa kupitia uwekezaji huo mkubwa zaidi ya ajira mpya 12,547
zimezalishwa kutokana na Benki kufadhili miradi ya muda wa kati na mrefu nchini.

“Tunajivunia kutekeleza malengo ya Serikali kwa kuwekeza zaidi ya Shilingi 630.3 bilioni
katika miradi ya maendeleo ambazo zimezalisha zaidi ya ajira mpya 12,547,” amesema.

Ameongeza kuwa uwekezaji huu umegusa maeneo ya kipaumbele ya Serikali pamoja na
Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) hasa katika Shilingi 162.7 bilioni zimewekezwa
kuongeza usalama wa chakula na kupunguza njaa, Shilingi 4.3 bilioni zimewekezwa
kuboresha elimu kupitia miradi ya taasisi za elimu, Shilingi 22.4 bilioni zimewekezwa
katika upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kupitia miradi ya mamlaka za maji.

Uwekezaji mwengine ni Shilingi 11.5 bilioni zimewekezwa katika nishati safi na nafuu
kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification
Expansion Programme-TREEP), Shilingi 250.7 bilioni zimewekezwa katika ukuaji wa uchumi na ajira, ikihusisha sekta za utalii, viwanda, na usafirishaji na Shilingi 24.7 bilioni zimewekezwa kuboresha miji na makazi.

Akizungumzia mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Benki hiyo, Bibi Mbassy
amesema TIB kama benki ya maendeleo ni taasisi ya kisera ambayo ina jukumu la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa hususani kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo

“Katika mwaka 2025 Benki vipaumbele vyake vimejikita katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa ili kuongeza kasi ya maendeleo,
pamoja na kutekeleza vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kuwa Benki itaendelea kukuza mtaji wa Benki kwa kushirikiana na taasisi za
fedha za kimataifa ili kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo yenye athari Chanya kwa jamii na uchumi.

Kupitia mradi wa upanuzi wa nishati ya umeme vijijini (Tanzania Rural Electrification
Expansion Programme-TREEP), Benki inaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia kupitia REA, kutoa mikopo kwa wazalishaji wa nishati jadidifu wanaohudumia maeneo ya vijijini ambako umeme wa TANESCO haujafika.

Vilevile, Bibi Mbassy amesema Benki ya Maendeleo TIB itaendelea kushirikiana na
SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA MAENDELEO YA VIWANDA (UNIDO) katika
kuchochea matumizi ya ethano kama chanzo mbadala cha nishati safi na nafuu ya kupikia kupitia mradi wa ‘’waste to energy’’.

Pia, Benki itaendelea na uwekezaji kwenye mamlaka za Maji na Kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya ujenzi wa Makazi bora, Elimu, Utalii , Afya na upanuzi wa Bandari Kavu.

No comments:

Post a Comment